Dalili Za Hatari Kwa Mimba Changa.

Mimba changa inaweza kuwa na dalili tofauti kwa kila mwanamke na inaweza kutofautiana kulingana na wiki za ujauzito.

Hata hivyo, kuna dalili kadhaa za hatari ambazo zinaweza kutokea wakati wa mimba changa na zinapaswa kuchukuliwa kwa umakini.

mimba changa

Ikiwa una dalili hizi, ni muhimu kuwasiliana na daktari wako au kutafuta huduma ya matibabu haraka iwezekanavyo:

1) Kutokwa Na Damu Ukeni.

Kutokwa na damu sehemu za siri wakati wa ujauzito ni dalili inayoweza kuashiria tatizo kwenye mimba ambalo linapaswa kuchunguzwa na daktari.

2) Maumivu Ya Chini Ya Tumbo.

Maumivu makali au maumivu ya chini ya tumbo yanaweza kuwa dalili ya tatizo la mimba. Maumivu haya yanaweza kuambatana na kutokwa na damu au bila kutokwa na damu.

3) Maumivu Makali Ya Kifua.

Maumivu makali ya kifua yanapaswa kuchunguzwa kwa umakini, kwani yanaweza kuwa ishara ya tatizo la moyo au matatizo mengine ya kiafya yanayohitaji matibabu haraka.

4) Kichefuchefu Na Kutapika.

Ikiwa unapata kichefuchefu na kutapika sana, ambayo inaweza kusababisha upotevu mkubwa wa maji (severe dehydration), unapaswa kutafuta matibabu haraka ili kuzuia utapiamlo (malnutrition) na kuwa na mzunguko mzuri wa maji mwilini.

5) Maumivu Ya Mgongo Au Kichwa.

Maumivu ya mgongo au kichwa ya mara kwa mara haswa yakiambatana na kutokwa na damu au shinikizo la juu la damu, yanaweza kuwa ishara ya matatizo ya afya wakati wa ujauzito.

6) Kupoteza Fahamu Au Kuzirai.

Kupoteza fahamu au kuzirai kunaweza kuashiria matatizo makubwa ya afya wakati wa mimba.

Soma pia hii makala: Kifafa Cha Mimba: Vijue Visababishi, Dalili, Matibabu, Madhara Yake Na Jinsi Ya Kuepuka.

7) Mabadiliko Ya Kasi Ya Mapigo Ya Moyo.

Ikiwa unaona kuwa mapigo ya moyo yameongezeka sana au kushuka sana, hii inaweza kuwa ishara ya tatizo la moyo au shinikizo la juu la damu damu.

HITIMISHO:

Ni muhimu kutambua kuwa dalili hizi za hatari zinaweza kuwa ishara ya matatizo yanayohitaji matibabu haraka ili kulinda afya yako na afya ya mtoto wako.

Ikiwa una hofu au wasiwasi wowote kuhusu hali yako wakati wa mimba, usisite kumwambia daktari wako au kutafuta huduma ya matibabu mara moja. Daktari ataweza kuchunguza hali yako na kutoa ushauri na matibabu sahihi.

Lakini pia, kwa uhitaji wa updates, vitabu (e-booksbure kuhusu afya jisajili (subscribe) kupitia email yangu kwa kubonyeza hii link: https://isayafebu.beehiiv.com/subscribe

vipimo vya mfumo wa uzazi