Ndiyo, Beetroot Inaongeza Damu!


Beetroot Inasaidia Nini?
Beetroot ni mojawapo ya vyakula bora kwa kuongeza damu, hasa kwa mjamzito. Hii ni kwa sababu ina:
1) Madini Ya Chuma (Iron).
Beetroot ni chanzo kizuri cha madini ya chuma, ambayo husaidia katika utengenezaji wa seli nyekundu za damu na kuzuia upungufu wa damu (anemia), tatizo linaloathiri wanawake wengi hasa wakati wa hedhi au ujauzito.


2) Foliki Asidi (Folate).
Beetroot ni chanzo kizuri cha folate, ambayo ni muhimu sana wakati wa ujauzito katika utengenezaji wa seli nyekundu za damu. Folate pia husaidia kuzuia kasoro za mfumo wa neva (neural tube defects) kwa watoto wachanga. Wanawake wajawazito wanashauriwa kutumia beetroot ili kuhakikisha wanapata kiwango cha kutosha cha folate.


3) Vitamin C.
Beetroot ni chanzo kizuri cha vitamini C ambayo husaidia mwili kufyonza madini ya chuma kwa ufanisi zaidi.

HITIMISHO:
Kwa ujumla, beetroot ni chakula cha asili chenye faida nyingi kwa mwanamke na kinaweza kuchangia afya bora ikiwa kitatumiwa mara kwa mara katika mlo wa kila siku. Kwa matokeo mazuri, inashauriwa kutumia beetroot safi, iwe kama juisi, saladi, au mboga iliyoandaliwa vizuri.
Leave a Reply