Faida Za Kufanya Mapenzi Kwa Mjamzito.

Kwa kawaida, kufanya mapenzi wakati wa ujauzito ni salama kwa wanawake wengi ikiwa ujauzito wao hauna matatizo. Wanandoa wengi wanaendelea kufurahia uhusiano wa kimapenzi wakati huu, ingawa mabadiliko ya kimwili na kihisia yanaweza kuathiri tamaa na faraja wakati wa kitendo hicho.

Tendo La Ndoa
Kufanya Mapenzi

Leo katika mada yetu ya blogu hii tutazungumzia baadhi ya faida za kufanya mapenzi kwa mjamzito. Ungana nami katika kuchambua faida hizi.

1) Kupunguza Msongo Wa Mawazo.

Kufanya mapenzi wakati wa ujauzito huchochea utolewaji wa homoni za furaha kama vile endorphins na oxytocin, ambazo hupunguza msongo wa mawazo (stress) na kuleta hisia za furaha. Hii humsaidia mjamzito kujisikia vizuri hali ambayo huboresha uhusiano na mwenza wake.

2) Kuboresha Mzunguko Wa Damu.

Kufanya mapenzi kunaweza kusaidia kuboresha mzunguko wa damu, jambo ambalo ni muhimu wakati wa ujauzito. Mzunguko mzuri wa damu husaidia kusafirisha virutubisho kwa mtoto aliye tumboni na kuboresha afya ya mama.

3) Kuimarisha Mfumo Wa Kinga Ya Mwili.

Kufanya mapenzi mara kwa mara kunaweza kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili kwa kuongeza uzalishaji wa antibodies kama vile immunoglobulin A (IgA), ambayo husaidia mwili kupambana na maambukizi. Hii ni muhimu hasa kwa mjamzito ili kumlinda yeye na mtoto aliyetumboni.

4) Kuboresha Usingizi.

Wanawake wajawazito mara nyingi hukumbwa na matatizo ya usingizi kutokana na mabadiliko ya homoni na mwili. Baada ya kufika kileleni (orgasm), baadhi ya wanawake hupata usingizi mzuri kutokana na homoni kama vile oxytocin na prolactin zinazozalishwa.

5) Kuimarisha Misuli Ya Nyonga (Pelvic Floor Muscles).

Kufanya mapenzi husaidia kuimarisha misuli ya nyonga, ambayo ni muhimu kwa ajili ya kumsaidia mwanamke mjamzito wakati wa kujifungua.

6) Kuboresha Uhusiano Wa Kimapenzi.

Wakati wa ujauzito, kufanya mapenzi kunaweza kusaidia kudumisha ukaribu wa kihisia kati ya wenza. Mabadiliko ya mwili na homoni yanaweza kuathiri hisia za mwanamke, lakini kufanya mapenzi kwa upendo kunaweza kusaidia kuimarisha uhusiano.

7) Kupunguza shinikizo la damu.

Baadhi ya tafiti zimeonyesha kuwa kufanya mapenzi kunaweza kusaidia kupunguza shinikizo la damu kwa muda mfupi, jambo ambalo ni muhimu kwa mjamzito ili kuzuia matatizo kama vile kifafa cha mimba (pre-eclampsia)

8) Kuchochea Maandalizi Ya Mwili Kwa Ajili Ya Kujifungua.

Kusisimka na kufika kileleni wakati wa kufanya mapenzi kunaweza kuchochea mikazo midogo ya misuli ya mji wa mimba (braxton hicks contraction). Hii siyo hatari kwa mwanamke mwenye ujauzito wenye afya, bali inasaidia mwili kujiandaa kwa kujifungua kwa namna ya kawaida (spontaneous vaginal delivery). Pia, shahawa za mwanaume zina prostaglandins, ambazo zinaweza kusaidia katika kulainisha (ripening) mlango wa kizazi kwa ajili ya leba wakati unapokaribia kujifungua.

Mikao ya kushiriki tendo la ndoa (sex positions) inayoshauriwa kutumika kwa mjamzito.

sex positions for pregnant women

HITIMISHO:

Ingawa kuna faida nyingi za kufanya mapenzi wakati wa ujauzito, ni muhimu kuzingatia usalama wa afya ya mjamzito. Unapopata dalili kama vile kutokwa na damu ukeni (per vaginal bleeding), maumivu makali wakati wa tendo la ndoa (dyspareunia), au matatizo yoyote wakati wa kufanya mapenzi, ni vyema kumwona daktari. Pia, baadhi ya hali za kiafya, kama vile placenta previa, zinaweza kumfanya mjamzito asifanye mapenzi kwa usalama wake na wa mtoto aliyetumboni.