Dalili Za UTI Sugu Kwa Mwanamke.

UTI Sugu:

UTI sugu (chronic uti) ni hali ambapo maambukizi ya njia ya mkojo hujirudia mara kwa mara au yanaendelea kwa muda mrefu licha ya matibabu ya awali.

UTI sugu ni tatizo kubwa zaidi ya UTI ya kawaida na inaweza kusababisha madhara makubwa endapo haitatibiwa ipasavyo.

Dalili za UTI sugu kwa mwanamke zinaweza kuwa na mfanano na zile za maambukizi ya kawaida ya njia ya mkojo, lakini zinadumu kwa muda mrefu au kujirudia mara kwa mara.

Mfumo Wa Mkojo Wa Mwanamke:

uti

Dalili za uti sugu kwa mwanamke ni pamoja na;

1) Maumivu Wakati Wa Kukojoa.

Mwanawake anaweza kuhisi maumivu makali au hisia ya kuchoma (burning sensation) wakati wa kukojoa, hali hii inajulikana kama dysuria.

2) Kuhisi Haja Ya Kukojoa Mara Kwa Mara.

Hali hii inajulikana kama polyuria, ambapo mwanamke anahisi haja ya kukojoa mara kwa mara hata kama mkojo ni kidogo.

3) Mkojo Wenye Harufu Mbaya Au Wenye Rangi Isiyo Ya Kawaida.

Mkojo unaweza kuwa na harufu kali au rangi ya mawingu (cloud colour).

4) Kukojoa Damu.

Mkojo unaweza kuwa na damu au kuwa na rangi ya waridi/mwekundu hali inayojulikana kama hematuria.

5) Maumivu Ya Tumbo Chini Ya Kitovu.

Mwanawake anaweza kuhisi maumivu ya tumbo chini ya kitovu ambayo yanaweza kuambatana na maumivu ya nyonga.

6) Maumivu Ya Mgongo.

Hii inaweza kuwa dalili kwamba maambukizi yameenea hadi kwenye figo.

7) Maumivu Wakati Wa Tendo La Ndoa.

UTI sugu inaweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa hali inayojulikana kama dyspareunia.

8) Uchovu Wa Kudumu.

UTI sugu inaweza kusababisha uchovu usio wa kawaida au hisia za kutojisikia vizuri muda wote.

9) Homa.

Ingawa si kila mara, UTI sugu inaweza kuambatana na homa na wakati mwingine baridi.

Kwa elimu zaidi kuhusu UTI kwa wanawake soma hapa: Uti Kwa Wanawake: Zijue Sababu 3 Zinazopelekea Kuugua Uti, Tiba Mbadala Na Jinsi Ya Kujikinga.

HITIMISHO:

Ikiwa mwanamke ana dalili hizi kwa muda mrefu au zinaendelea kujirudia licha ya matibabu, anaweza kuwa na UTI sugu, na inashauriwa kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi na matibabu maalum.