Masundosundo Sehemu Za Siri.

Masundosundo Ni Nini?

Masundosundo ni vinyama vidogo vinavyoota katika maeneo ya sehemu za siri, vinyama hivyo vinaweza kutokea kwenye uume, uke, mrija wa mkojo (urethra), vulva, shingo ya kizazi (cervix), au maeneo ya kuzunguka njia ya haja kubwa au ndani yake, ni ugonjwa unaoenezwa kwa njia ya kujamiiana.

Masundosundo pia hujulikana kwa kitaalamu kama Genital warts.

Ugonjwa huu husambazwa kwa mgusano wa ngozi kwa ngozi hasa wakati wa ngono, japo migusano mingine ya maeneo athirika isiyohusisha ngono inaweza pia kuwa chanzo cha kusambaa kwake.

Mara baada ya kuambukizwa, ugonjwa huu huweza kuchukua mpaka muda wa wiki sita hadi miezi 6 kwa masundosundo kuwa dhahiri, ingawa baadhi ya wagonjwa wanaweza kukaa hata miaka kadhaa bila kuwa na dalili yoyote ile.

Kisababishi Cha Masundosundo:

Masundosundo husababishwa na virusi wajulikanao kwa kitaalamu kama Human papilloma virus (HPV). 

Ripoti ya shika la afya duniani (WHO) zinasema kwamba kuna aina zaidi ya 100 ya virusi wa papilloma waliokwisha kugunduliwa mpaka sasa ambapo kati ya hao ni aina mbili tu, HPV-6 na HPV-11 ambao ndio husababisha masundosundo.

hpv

Tabia Hatarishi Zinazosababisha Masundosundo:

Zifuatazo ni tabia hatarishi zinazomuweka mtu katika hatari ya kupata masundosundo ambazo ni pamoja na;

1) Kuwa Na Wapenzi Wengi.

Ikiwa una wapenzi wengi (multiple sexual partners) na hautumii kinga (condom) wakati wa kushiriki ngono basi unajiweka katika hatari ya kupata masundosundo.

2) Kufanya Ngono Isiyo Salama Na Mwathirika Wa Masundosundo.

Ikiwa unashiriki ngono isiyo salama na mtu aliyeathirika na virusi wa Hpv basi unajiweka katika hatari kubwa ya kupata masundosundo.

3) Ngono Katika Umri Mdogo.

Watu wanaoanza ngono mapema wapo kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata masundosundo kutokana na kinga za mwili kuwa chini sana.

4) Matumizi Makubwa Ya Sigara Na Pombe.

Tafiti zinaonesha kwamba watu wenye matumzi makubwa ya pombe na sigara wanajiweka katika hatari ya kupata masundosundo.

Kwa hiyo, ingawa uvutaji wa sigara na unywaji pombe si sababu za moja kwa moja za kupata masundosundo, tabia hizi zinaweza kudhoofisha kinga ya mwili na kuongeza hatari ya kuambukizwa HPV.

5) Upungufu Wa Kinga Mwilini (immunosuppression).

Kuwa na upungufu katika mfumo wa kinga mwilini kutokana na magonjwa mbalimbali kama vile kisukari, HIV, cancer au kwa sababu ya matumizi ya dawa fulani humuweka mtu katika hatari kubwa ya kupata masundosundo. Pia hali ya kuwa na lishe duni (malnutrition) husababisha kushuka kwa kinga ya mwili hivyo kupelekea mtu kuwa katika hatari ya kupata masundosundo.

6) Ujauzito.

Wakati wa ujauzito, mabadiliko ya homoni, mabadiliko katika mfumo wa kinga ya mwili yanaweza kuongeza uwezekano wa kupata masundosundo.

7) Kuchangia Vitu Binafsi Na Mwathirika Wa Masundosundo.

Kuchangia (kushea) vitu binafsi kama vile taulo, nguo za ndani, na vifaa vya usafi wa mwili vinavyotumiwa na mtu mwenye masundosundo vinaweza kuhamasisha kuenea kwa HPV na kusababisha masundosundo.

Dalili Za Masundosundo:

Masundosundo huonekana kama vioteo laini vinavyojitokeza juu ya ngozi ingawa wakati mwingine vinaweza kuwa vidogo mno kiasi cha kutoweza kuonekana vizuri kwa macho ya kawaida.

Kwa wanaume, vioteo hivi hutokea zaidi kwenye uume, ngozi ya pumbu, eneo la mitoki, mapajani pamoja na maeneo ya kuzunguka nje ya njia ya haja kubwa au ndani yake; wakati kwa wanawake hutokea ndani ya uke au njia ya haja kubwa, nje ya uke au ngozi ya nje kuzunguka njia ya haja kubwa, au ndani ya uke kuzunguka eneo la shingo ya kizazi.

Kwa wale wanaopenda kufanya ngono ya mdomoni (oral sex), wanaweza kupatwa na masundosundo kwenye maeneo ya kuzunguka mdomo (lips), kwenye ulimi na hata kwenye utando unaozunguka koo.

Dalili nyingine ya masundosundo ni kama vile mgonjwa kujihisi kukosekana kwa hisia (kufa ganzi) maeneo yaliyozungukwa na masundosundo.

kwa wanawake kuongezeka kwa utoko/ uchafu sehemu za siri, kuwashwa sana maeneo ya siri na wakati mwingine kutokwa na damu ukeni mara baada ya tendo la ngono. Hata hivyo dalili hizi hutokea mara chache sana.

Wanawake wengi vijana wanaojihusisha na vitendo vya ngono [sexually active] huambukizwa sana ugonjwa huu lakini wengi wao hupona bila hata kuhitaji matibabu, wakati wanaume wanaoambukizwa, wengi wao huwa hawaoneshi dalili zozote za ugonjwa ingawa wanaweza kuwaambukiza wenzi wao bila ya wao kujua.

Dawa Ya Masundosundo:

Mbali na matibabu ya masundosundo kufanyika hospitali kwa kuondoa vioteo juu ya ngozi iliyoathirika, matibabu mengine uhusisha matumizi ya dawa utakazoandikiwa na daktari na kuelekezwa namna ya kuzitumia mwenyewe nyumbani kwa siku kadhaa mpaka majuma kadhaa. 

Dawa zinazotumika ni pamoja na Podophyllin na podofiloxTrichloroacetic acid (TCA) au Imiquimod.

podophyllin cream

Soma pia hii makala: Jinsi Ya Kutumia Podophyllin.

Madhara Ya Masundosundo:

Kwa baadhi ya wagonjwa, masundosundo yanaweza kuwa mengi na makubwa sana kiasi cha kuhitaji matibabu ya muda mrefu na ghali zaidi pamoja na ufuatiliaji wa kina.

Jinsi Ya Kujikinga Na Masundosundo:

Njia mojawapo ya uhakika kabisa ya kujiepusha na masundosundo pamoja na magonjwa mengine ya ngono/zinaa ni kujiepusha na matendo ya ngono na zinaa kabisa. 

Lakini kwa wale ambao ni ngumu kufanya hivyo, wanaweza kupunguza uwezekano wa kupatwa na ugonjwa huu kwa kujihusisha kingono na mwenza mmoja tu ambaye una uhakika kuwa hajaambukizwa wala hayupo katika hatari ya kuambukizwa magonjwa haya.

Tofauti na magonjwa mengine ya zinaa, matumizi ya condom hayana uhakika wa asilimia mia moja katika kukukinga dhidi ya HPV kwa sababu virusi wa HPV au hata masundosundo yanaweza kuwa nje kwenye ngozi ambayo uwezekano wa kugusana ni mkubwa.

Pamoja na hayo, bado condom inaweza sana kupunguza hatari ya kuambukizwa masundosundo ikiwa tu itatumika vema na inashauriwa kuitumia mara zote unapokutana kingono na mwenza usiye na uhakika naye. Tukumbuke kila wakati kuwa HPV inaweza bado kuambukizwa kwa mtu hata kama mwenza hana masundosundo yanavyoonekana au hana dalili zozote zile. 

Ikiwa kuna uwezekano, ni vyema kwa wanawake wote wenye umri wa miaka kati ya 9 mpaka 26 kupata chanjo dhidi ya virusi wa HPV ili kuzuia uwezekano wa kuambukizwa virusi hao ambao hatimaye husababisha saratani ya shingo ya kizazi.

HITIMISHO:

Ikiwa utahitaji virutubisho kwa ajili ya kutokomeza changamoto ya kuota vinyama sehemu za siri, genital warts bonyeza hapa: “Jinsi Ya Kutibu Ugonjwa Wa Kuota Vinyama Sehemu Za Siri Bila Kufanya Upasuaji.”

Lakini pia, kwa uhitaji wa updates, vitabu (e-books) bure kuhusu afya jisajili (subscribe) kupitia email yangu kwa kubonyeza hii link: https://isayafebu.beehiiv.com/subscribe