Damu Ni Nini?
Damu ni tishu iliyo katika hali ya kimiminika mwilini ambayo imeundwa na seli nyekundu, seli nyeupe, chembe sahani na plazma. Vitu hivi vinavyounda damu hutengenezwa kwenye uroto unaopatikana ndani ya mifupa, uroto huo upo wa aina mbili, uroto wa njano/mweupe na uroto mwekundu. Uroto wa njano/mweupe unatengeneza seli nyeupe za damu lakini uroto mwekundu unatengeneza chembe sahani na seli nyekundu.
Seli nyekundu za damu ni seli za damu zenye rangi nyekundu na zina umbo la duara lililobonyea katikati, seli nyekundu huishi kwa wastani wa siku 120 au miezi minne au wiki 16. Baada ya hapo zinakufa na kubadilishwa na ini kuwa pigimenti za nyongo, pigimenti za nyongo kwanza zina kazi ya kumeng’enya fati na pili kukipa kinyesi rangi yake.
Seli nyekundu kwa kutumia haemoglobini iliyo ndani yake hubeba oksijeni kutoka kwenye mapafu na kuipeleka kwenye seli kuunguza chakula ili kutoa nishati, kisha hubeba kabonidayoksaidi kutoka katika seli na kuirudisha kwenye mapafu. Iwapo seli nyekundu zitabadili umbo lake la duara basi zitashindwa kubeba oksijeni na pia zitakwama kupita katika baadhi ya mishipa ya damu, hali ambayo hujulikana kwa kitaalamu kama sickle cell disease (SELIMUNDU).
seli nyeupe hazina umbo maalumu na zinafana sana na seli za mnyama. Kazi yake ni kuua/kupambana na vimelea vya magonjwa mwilini. Seli nyeupe katika harakati zake za kupambana na vimelea vya magonjwa huzidiwa na kufa ambapo zikifa hugeuka kuwa USAHA.
chembe sahani ni vipande vya seli nyekundu za damu, kazi yake ni kugandisha damu unapopata jeraha, hugandisha damu hiyo kwa kutumia Fibrinojeni iliyo katika chembe sahani hizo.
plazma ni maji ya damu, tunaweza kusema ni mto wa damu, plazma inafanya kazi ya kubeba chakula, homoni, uchafu, seli za damu na vyote vilivyomo kwenye damu.
Upungufu wa damu ni ile hali ya kiasi cha damu mwilini kuwa kidogo kuliko kinachotakiwa na mwili kulingana na hali ya mtu na jinsia yake. Hali hiyo hupimwa maabara na hospitali kwa kuangalia kiasi cha Haemoglobini (Hb).
Katika hali ya kawaida mwanaume hutakiwa kuwa na damu kati ya 13.5 hadi 17.5 (g/dl) na wanawake hutakiwa kuwa na damu kati ya 12.0 hadi 15.5 (g/dl) na kwa mjamzito kikawaida kiasi cha damu inatakiwa kuwa kati ya 11-12g/dl. Tofauti hiyo husadikiwa kwamba huletwa na hedhi ambayo wanawake hupata kila mwezi na hivyo kuwa na damu pungufu kidogo ukilinganisha na ya wanaume.
Leo katika mada yetu ya blogu hii tutazungumzia aina za vyakula vinavyosaidia kuongeza wingi wa damu mwilini.
Vyakula Vinavyoongeza Damu Kwa Wingi Mwilini:
Vifuatavyo ni vyakula vinavyosaidia kuongeza wingi wa damu katika mwili ambavyo ni pamoja na;
1) Mboga Za Majani.
Mboga za majani kama vile mchicha, spinach, na kale (leaf cabbage) zina kiwango kikubwa cha folate, madini ya chuma, na vitamini C ambavyo ni muhimu katika uzalishaji wa seli nyekundu za damu mwilini.
2) Nyama Nyekundu.
Nyama ya ng’ombe, nyama ya kondoo na aina nyingine ya nyama nyekundu ni chanzo muhimu cha madini ya chuma mwilini ambacho ni muhimu katika utengenezaji wa haemoglobini, sehemu ya seli nyekundu za damu.
3) Mbegu Za Maboga Na Karanga.
Mbegu za maboga na karanga zina kiwango kikubwa cha madini ya chuma, folate na vitamini E ambavyo vinaweza kusaidia kuongeza kiwango cha damu mwilini.
4) Matunda.
Matunda kama vile embe, nanasi, zabibu, chungwa, nyanya yana kiwango kikubwa cha vitamini C ambayo husaidia mwili kuchukua madini ya chuma vizuri zaidi na hivyo kuongeza kiwango cha damu mwilini.
5) juisi.
Sio juisi zote huongeza kiwango cha damu, unashauriwa kunywa juisi ya nyanya, walau kila siku glasi mbili lakini pia juisi za rozella, tikitimaji na karoti. Aina hizi za juisi huongeza kiwango cha damu kuliko hata vidonge.
6) Mchele Mweupe.
Mchele mweupe una kiwango kikubwa cha madini ya chuma ambacho ni muhimu katika utengenezaji wa seli nyekundu za damu na hivyo kuongeza kiwango cha damu mwilini.
Soma pia hizi makala:
Dalili Za Kupungukiwa Damu Kwa Mama Mjamzito:
Mama mjamzito unapohisi dalili zifuatazo ni vizuri kupima wingi wa damu, kwani kiasi cha damu kinatakiwa kisiwe chini ya 11g/dl mpaka mama unapoenda kujifungua.
Dalili za upungufu wa damu kwa mama mjamzito ni pamoja na;
1) Kuchoka sana, japo kuchoka sana ni hali ya kawaida kwa mama mjamzito, hivyo unapoona unachoka sana ni vizuri kwenda kuangalia wingi wa damu.
2) kukosa pumzi.
3) Kizunguzungu.
4) Maumivu makali ya kichwa.
5) Miguu kuishiwa nguvu.
6) Midomo kupauka.
Kumbuka:
Japo dalili nyingine zinaweza kuwa za kawaida lakini unapopata dalili zisizo za kawaida wahi kituo cha afya kupata vipimo na ushauri.
Vyakula Vinavoongeza Damu Kwa Mjamzito:
Vifuatavyo ni vyakula vinavyosaidia kuongeza kiwango cha damu kwa mjamzito ambavyo ni pamoja na;
1) Heme Iron Foods.
Hivi ni vyakula ambavyo vina kiwango kikubwa cha madini ya chuma (iron minerals)) na mwili huweza kuchukua madini yake ya chuma kirahisi.
Mfano wa vyakula hivi ni pamoja na nyama nyekundu, samaki, nyama ya kuku, maini na dagaa.
2) Non Heme Iron Foods.
Hivi ni vyakula ambavyo vina madini ya chuma (iron minerals) ya kutosha ila mwili hauwezi kuyachukua kirahisi hivyo basi unapokula vyakula hivi jitahidi kula na vyakula vyenye vitamin C kama vile machungwa, mapapai, nyanya na pilipili hoho ili uhusaidie mwili kuyachukua madini hayo kwa urahisi.
Mfano wa vyakula hivi ni pamoja na beetroot, mboga za majani zote hasa matembele na spinach.
Juice ya tembele na passion husaidia kuongeza damu kwa haraka hasa kwa wale ambao beetroot imewashinda , hii juice inaongeza damu kwa haraka sana.
Jinsi Ya Kuandaa Juisi Ya Tembele Na Passion.
Osha matembele yako kwenye maji ya vuguvugu kuondoa uchafu ukimaliza yakate Kate kisha weka kwenye blender na mbegu za passion saga na maji, ukimaliza chuja juice yako japo unaweza kunywa hivyo hivyo au ukaongezea sukari. Unaweza changanya na ubuyu mweupe, ubuyu mweupe utatumia juice yake badala ya passion. Kunywa Mara mbili kwa siku kadri uezavyo ladha yake ni nzuri huwezi shidwa tumia.
Vyakula vingine vinavyosaidia kuongeza kiwango cha damu kwa mjamzito ni pamoja na: Mayai ya kienyeji, viazi vitamu, tende unaweza changanya na maziwa fresh, viazi mbatata, maharage, njegere, karanga, almond, mbegu za maboga, kunde chemsha kunywa maji yake au supu yake.
Kumbuka:
Unapokula vyakula vyenye madini ya chuma usinywe pamoja na chai, kahawa au soya kwani huzuia mwili kuyachukua madini hayo kwa urahisi (impair iron absorption).
Dawa Za Kuongeza Damu Kwa Haraka:
Ikiwa unahitaji kuongeza damu kwa haraka basi unashauriwa kutumia dawa zilizotengenezwa kutokana na mimea na matunda ambazo ni pamoja na;
1) Carotenoid complex.
Hii ni mojawapo ya dawa ambayo inasaidia kuongeza damu mwilini kwa haraka, dawa hii ina jumla ya vidonge 90.
2) Multi Neolife.
Hii pia ni mojawapo ya dawa ambayo inasaidia kuongeza damu mwilini kwa haraka, dawa hii ina jumla ya vidonge 30.
HITIMISHO:
Upungufu wa damu hutokana na kupungua kwa madini ya chuma mwilini, hivyo unashauriwa kutumia vyakula vilivyotajwa hapo juu ili kuongeza kiwango cha damu mwilini na kuondokana na changamoto ya upungufu wa damu mwilini.
Lakini pia kama utahitaji dawa zilizotajwa hapo juu kwa ajili ya kuongeza damu mwilini kwa haraka wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487.
Kwa uhitaji wa updates, vitabu (e-books) bure kuhusu afya jisajili (subscribe) kupitia email yangu kwa kubonyeza hii link: https://isayafebu.beehiiv.com/subscribe
Ni mimi mwenye kujali afya yako Dr. Isaya Febu.
Je Unasumbuliwa Na PID, Fangasi Sugu Au UTI Sugu Kwa Muda Mrefu Bila Kupata Suluhisho La Uhakika?
Kiasi ambacho umeshajikatia tamaa na huelewi ufanye nini ili kutatua changamoto yako inayokunyima usingizi?
Kama jibu ni NDIYO, basi usiwe na wasiwasi kwani nimekuletea suluhisho la changamoto yako…
Huhitaji kuendelea kutumia dawa za mahospitali ambazo umekuwa ukitumia kwa muda mrefu bila kupona…
Suluhisho halisi kwa changamoto yako aidha ni PID, FANGASI SUGU au Uti sugu utalipata kupitia kitabu (soft copy) kitakachokupa muongozo wa kujitibia changamoto yako uwapo mazingira ya nyumbani kwako…
Gharama ya kitabu hicho mara zote ni TZS 10,000/= ila kwa kuwa leo hii ni sherehe ya kumbukizi ya siku yangu ya kuzaliwa (birthday) nitakupatia kwa bei ya OFA ya TZS 3000/= tu (okoa 7,000/= nzima)…
Ili Kupata OFA hiyo Lipia kwenda Tigo Pesa namba 0653211873 (Isaya Febu Msemwa) Kisha nitumie muamala wako WhatsAPP Kwa kubonyeza hapa: https://wa.me/+255625305487
PS: Ofa hii itaisha kesho saa 6:00 mchana, weka oda yako mapema Kwani ukiikosa leo, kuipata tena mpaka mwakani tarehe kama ya leo.
Vipi kuhusu maziwa ya ng’ombe je yanaongeza damu pia? Asante