Ni kawaida kwa wanaume wengi kushuhudia uume “kulala” au kulegea mara tu baada ya kumaliza tendo la kwanza la ngono (kufika kileleni / kumwaga shahawa).
Hali hii husababishwa na mabadiliko ya kimwili na homoni baada ya kufika kileleni (kumwaga shahawa). Lakini kwa wanaume wengine, inaweza kuwa changamoto iwapo wanatamani kuendelea na mzunguko wa pili wa tendo.
Hivyo basi, hali hii haimaanishi tatizo la kiafya moja kwa moja, bali inaweza kuwa ya kawaida kulingana na mwili wa mwanaume, umri, na afya kwa ujumla.

Leo katika mada yetu ya blogu hii tutazungumzia sababu kadhaa zinazoweza kusababisha uume kulala haraka baada ya bao la kwanza na njia za kusaidia kuongeza nguvu kwa mwanaume baada ya bao la kwanza. Ungana nami katika somo hili.
1) Kipindi Cha Kurejea (Refractory Period).
Baada ya mwanaume kufika kileleni (ejaculation), mwili huingia kwenye kipindi cha kupumzika kinachoitwa refractory period ambapo huwezi tena kupata msisimko wa haraka. Kipindi hiki huchukua dakika chache hadi saa kadhaa, kulingana na umri na afya ya mwanaume.

2) Kuchoka Kwa Mwili/Akili.
Uchovu wa kimwili au kiakili kutokana na shughuli nyingi kabla ya tendo la ndoa kunaweza kuathiri nguvu ya kurudia bao la pili.
3) Msongo Wa Mawazo (Stress).
Hofu, wasiwasi, au msongo wa mawazo huathiri uwezo wa kusimama tena kwa uume baada ya kumaliza bao la kwanza.

4) Kujichua Kupita Kiasi.
Wanaume wanaojichua mara kwa mara (punyeto) hupata mshuko wa haraka zaidi na uume kulala haraka baada ya kumwaga.

5) Lishe Duni Na Mzunguko Hafifu Wa Damu.
Ukosefu wa virutubisho muhimu kama vile zinki, uzito kupita kiasi, au presha ya damu isiyo sawa huathiri uwezo wa uume kusimama tena baada ya kumaliza bao la kwanza.


6) Kutokuwepo Na Mvuto Wa Kutosha Wa Kimapenzi Kwa Mpenzi Baada Ya Bao La Kwanza.
Hii pia ni mojawapo ya sababu za kisaikolojia zinazoweza kufanya uume kulala haraka baada ya bao la kwanza na mwanaume kushindwa kuendelea na round ya pili wakati wa tendo la ndoa.
Homoni ya Dopamine na Oxytocin, ambazo hujenga “muunganiko wa kimapenzi”, huweza kupungua ghafla endapo mwanaume hakuhusishwa kihisia sana.
Dalili za kutopata mvuto baada ya bao la kwanza ni pamoja na: Kukosa hamu ya kumgusa au kumkumbatia mwenza baada ya tendo, kutamani kutoka au kulala tu baada ya kumwaga.
7) Kukaa Muda Mrefu/Kutokuwa Na Mazoea Ya Kushiriki Tendo La Ndoa Mara Kwa Mara.
Ikiwa tendo la ndoa halijafanywa kwa muda mrefu sana au halifanywi mara kwa mara, mwili hauwezi kuzoea “stamina” ya kurudia tendo mara kadhaa.
Je, Hali Hii Ni Ya Kawaida?
Ndiyo. Kwa wanaume wengi, kupumzika baada ya bao la kwanza ni kawaida. Wanawake wanaweza kurudi kwenye msisimko haraka, lakini wanaume huhitaji muda zaidi wa kurejea. Hali hiyo inakuwa tatizo kwa mwanaume endapo:
- Uume unalala kabla ya kufika kileleni
- Uume hausimami kabisa hata baada ya muda
- Hali hii imekuwa ya mara kwa mara kwa muda mrefu na imeathiri mahusiano au ndoa yako
- Unakosa hamu ya tendo kabisa
Kumbuka: Kadri mwanaume anavyozidi kuzeeka, muda wa kupumzika baada ya bao huongezeka. Kwa vijana, inaweza kuwa dakika 5–15, kwa wazee inaweza kuwa hata zaidi ya saa.
Namna Ya Kurejesha Nguvu Baada Ya Bao La Kwanza:
Njia za kusaidia kuongeza nguvu kwa mwanaume baada ya bao la kwanza ni pamoja na:
1) Pata Muda Wa Kupumzika Baada Ya Bao La Kwanza.
Chukua muda kupumzika baada ya bao la kwanza kwani msukumo wa kurudia tendo haraka unaweza kufanya usifanikiwe. Ongea na mwenza wako, tenga muda mfupi, halafu endelea kwa raundi nyingine.

2) Tumia Muda Wa Kuamsha Tena Hisia (Foreplay).
Mfano: Busu, massage, kugusana kimahaba na mpenzi wako.

3) Kula Lishe Bora.
Vyakula kama parachichi, korosho, mbegu za maboga, karanga, asali, mayai na ndizi husaidia kuongeza stamina ya tendo la ndoa.

4) Fanya Mazoezi Ya Viungo (Pelvic Floor Exercise).
Mazoezi ya viungo, Kegel exercises ni mazoezi ya misuli ya nyonga yanayosaidia kuongeza nguvu ya uume na uwezo wa kudhibiti mshindo wa bao.

Tazama hapa jinsi ya kufanya kegel exercise: https://www.youtube.com/shorts/fXYOaAxxtws
5) Epuka Punyeto Kupita Kiasi.
Punyeto kupita kiasi huweza kupunguza hamu na uwezo wa kurudia tendo kwa wanaume.

6) Epuka Matumizi Ya Sigara Na Pombe Kupita Kiasi.
Matumizi ya sigara na pombe kupita kiasi inaathiri mishipa ya damu inayosababisha uume kusimama.

HITIMISHO:
Ukihitaji ushauri wa kitaalamu juu ya kuongeza uwezo wa kurudia bao au kurefusha muda wa uume kusimama, tunaweza kukusaidia kwa njia ya lishe, mazoezi na ushauri wa kitabibu.
Wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487, tukutakie siku njema.
Leave a Reply