Kupiga Punyeto:
Punyeto (kujichua) ni kitendo cha kusisimua kiungo cha uzazi (uume/uke) kwa kutumia kitu tofauti na kiungo cha uzazi kwa lengo la kujiridhisha kingono.

Madhara Ya Punyeto:
Ikiwa kitendo hicho kitafanyika mara kwa mara na ikawa ni tabia huchangia madhara kwa mwanaume na mwanamke ambapo kwa mwanaume, punyeto inaathiri uimara wa misuli ya uume na kupunguza uwezo wa kushiriki ngono kiasi cha kumridhisha mwenzi wako ipasavyo.
Kwa upande wa mwanamke, punyeto inakupunguzia uwezo wa kufurahia ngono katika hali ya kawaida kiasi ambacho unakuwa huwezi kupata msisimko wa kingono kwa urahisi hali inayopelekea kushindwa kufika kileleni katika tendo halisi la ndoa.
Kama ilivyo kwa tabia zingine hatarishi zinazochangia uraibu mfano uvutaji wa sigara na matumizi ya pombe kupita kiasi, tabia ya kupiga punyeto hupelekea uraibu pia kwa mhusika.
Punyeto Inaweza Kusababisha Ugumba Kwa Mwanaume?
Kupiga punyeto hakusababishi ugumba kwa mwanaume kwani hakuathiri moja kwa moja kiwanda cha kuzalisha mbegu za uzazi, mwili wa mwanaume huzalisha mbegu mpya za kiume (sperm) kila siku, hivyo hata kama mwanaume anapiga punyeto mara kwa mara, haitamaliza mbegu zake kabisa.


Leo ukiacha kupiga punyeto, ukala lishe bora, ukaacha unywaji wa pombe kupita kiasi na uvutaji wa sigara, ukafanya mazoezi hasa kegel exercise, mbegu mpya za kiume zinazalishwa za kutosha kiasi ambacho kufikia angalau miezi 3 unakuwa na uwezo mzuri wa kumudu tendo la ndoa kwa muda mrefu na kuzalisha.
Kwa hiyo, punyeto kwa wanaume inaathiri zaidi misuli ya uume jambo ambalo linapelekea misuli hiyo kuwa legevu kiasi ambacho huchangia mwanaume kupata tatizo la kuwahi kufika kileleni (premature ejaculation).
Punyeto Inaweza Kusababisha Ugumba Kwa Mwanamke?
Kupiga punyeto hakusababishi ugumba moja kwa moja kwa wanawake.
Japokuwa, kulingana na namna mwanamke anavyofanya kitendo hicho hasa vitu anavyotumia vinaweza kuwa sio salama vikaharibu via vya uzazi au kupelekea kupata maambukizi kwenye mfumo wa uzazi yajulikanayo kwa kitaalamu kama Pelvic Inflammatory Disease (PID) ambayo yakasababisha ugumba kama hayatatibiwa mapema, lakini moja kwa moja kitendo chenyewe hakisababishi ugumba kwa mwanamke.


HITIMISHO:
Kwa ujumla, punyeto haiwezi kusababisha ugumba kwa mwanaume au mwanamke isipokuwa kama kuna tatizo lingine la kiafya, kama vile maambukizi kwenye mfumo wa uzazi au matatizo ya homoni.
Leave a Reply