Kipimo Cha Mbegu Za Kiume.

Kipimo cha mbegu za kiume kinachojulikana kwa kitaalam kama “Semen Analysis” ni uchunguzi wa maabara unaotumika kupima ubora na afya ya shahawa za mwanaume. 

Hii ni moja ya vipimo muhimu sana katika kutathmini uwezo wa mwanaume kupata mtoto (fertility).

Kipimo hiki hutolewa kwa kuchukua sampuli ya manii, ambayo mwanaume anakusanya kwa njia ya kujichua, kisha sampuli hiyo hupimwa maabara.

mbegu za kiume

Vitu Vinavyopimwa Kwenye Kipimo Cha Mbegu Za Kiume:

Vifuatavyo ni vitu vinavyopimwa kwenye kipimo cha mbegu za kiume:

1) Kiasi Cha Shahawa (Volume).

  • Kawaida: 1.5 – 6 ml kwa utoaji mmoja.
  • Kiasi kidogo sana (<1.5 ml) kinaweza kuashiria tatizo la uzalishaji au kuziba kwa mirija ya mbegu.

2) Rangi Na Muonekano.

  • Kawaida: rangi nyeupe au kijivu hafifu.
  • Rangi isiyo ya kawaida (njano, kahawia, yenye damu) inaweza kuashiria maambukizi au matatizo ya kiafya kwenye mfumo wa uzazi wa mwanaume.

3) Muda Wa Kutanuka (Liquefaction Time).

  • Shahawa huanza kuwa nzito kisha hubadilika kuwa maji baada ya dakika 20–30.
  • Kutojitanua kunaweza kuathiri uhamaji wa mbegu.

4) Idadi Ya Mbegu (Sperm Count / Concentration).

  • Kawaida: angalau 15 milioni kwa ml au zaidi.
  • Chini ya hapo, hali hiyo huitwa oligospermia (mbegu chache)

5) Umbo La Mbegu (Morphology).

  • Kawaida: angalau 4% au zaidi ya mbegu ziwe na umbo la kawaida.
  • Umbo lisilo la kawaida linaweza kupunguza uwezo wa kurutubisha yai (mbegu zenye maumbo yasiyo ya kawaida haziwezi kurutubisha yai kwa ufanisi).

6) Uhai Wa Mbegu (Viability).

  • Zaidi ya 58% ya mbegu zinapaswa kuwa hai.

7) pH Ya Shahawa.

  • Kawaida: 7.2 – 8.0
  • Ikiwa chini sana au juu sana inaweza kuashiria maambukizi au tatizo la tezi za uzazi.

8) Uwezo Wa Kuogelea (Motility).

  • Angalau 40% ya mbegu zinapaswa kuwa na uwezo wa kuogelea (kusogea mbele) vizuri.
  • Zisipokuwa na uwezo wa kuogelea vizuri, hali hiyo huitwa asthenospermia.

9) Wbc (Seli Nyeupe).

  • Ikiwa seli nyeupe za damu zipo nyingi, huashiria uwepo wa maambukizi.

Mwanaume anashauriwa kuepuka kujamiana au kutoa mbegu angalau kwa saa 24 hadi 72 kabla ya kuchukua sampuli ili kupata matokeo sahihi. Pia, anatakiwa kuepuka matumizi ya pombe, kahawa na dawa za kulevya, na kuhakikisha anakuwa katika hali nzuri ya kimwili na kiakili kabla ya kipimo.

HITIMISHO:

Kipimo hicho kinapotolewa hutoa taarifa za kiwango, ubora na mwendokasi wa mbegu, hivyo kusaidia kubaini matatizo kama vile ugumba au ubora duni wa mbegu na kuchangia matibabu sahihi.