Zijue Dalili Za Uti.

Uti ni maambukizi yanayoathiri njia ya mkojo.

Dalili za uti zinaweza kutofautiana kulingana na sehemu ya mfumo wa mkojo ilioathiriwa (kama vile kibofu cha mkojo, urethra, au figo) na kwa kiwango cha maambukizi.

Zifuatazo ni dalili za kawaida za uti ambazo ni pamoja na:

1) Kukojoa Mara Kwa Mara.

Moja ya dalili za kawaida za uti ni haja ya kukojoa mara kwa mara.

Hii inaweza kuambatana na hisia ya kuchoma au kuwaka wakati wa kukojoa.

2) Maumivu Kwenye Sehemu Ya Chini Ya Tumbo.

Unaweza kuhisi maumivu au joto kwenye eneo la chini la tumbo, haswa karibu na mfupa wa nyonga.

3) Haja Ya Kukojoa Mara Kwa Mara Usiku.

 Watu wenye uti mara nyingi wanahisi haja ya kukojoa usiku hali inayojulikana kwa kitaalam kama Nocturia, ambayo inaweza kuvuruga usingizi wao.

4) Kukojoa Kidogo Kwa Kila Wakati.

Wakati mwingine, unaweza kuhisi kama unahitaji kukojoa sana, lakini unapokwenda kwenye choo, unatoa kiasi kidogo cha mkojo.

5) Mkojo Mweusi Au Una Harufu Mbaya.

Mkojo unaweza kubadilika rangi kuwa giza au una harufu mbaya kutokana na uwepo wa maambukizi.

6) Maumivu Ya Chini Ya Mgongo. 

Kwa baadhi ya watu, uti unaweza kusababisha maumivu ya chini ya mgongo au upande wa chini wa mwili kama ishara ya maambukizi ya figo.

7) Kichefuchefu Na Kutapika.

Baadhi ya watu wanaweza kuwa na kichefuchefu au kutapika kama matokeo ya uti, haswa ikiwa maambukizi yamefika kwenye figo.

8) Kuhisi Udhaifu Au Uchovu.

Uti inaweza kusababisha hisia za udhaifu au uchovu.

Soma pia hii makala: Zijue Dalili Za Uti Sugu.

HITIMISHO:

By the way, hivi unajua kwamba dawa asilia iitwayo PANACEA natural product itakusaidia kutokomeza kabisa changamoto ya uti?. Ndio ni kweli kupata dawa hii tuma ujumbe sasa hivi kwenda 0625 305 487.