Kitunguu Maji:
Kitunguu maji kimekuwa kikitumika kwa miaka mingi kama tiba ya asili kwa kuongeza nguvu za kiume na afya ya uzazi kwa wanaume. Kinachofanya kitunguu kuwa na nguvu hii ni kwa sababu ya kemikali asilia na virutubisho vilivyomo ndani yake.

Faida Za Kitunguu Maji Kwa Nguvu Za Kiume:
Faida za kitunguu maji kwa nguvu za kiume ni pamoja na:
1) Huchochea Uzalishaji Wa Homoni Ya Testosteroni.
Tafiti zinaonyesha kitunguu maji huchochea ongezeko la homoni ya kiume iitwayo testosteroni inayohusiana moja kwa moja na hamu ya tendo la ndoa (libido) na nguvu za kiume.

2) Huboresha Mzunguko Wa Damu Mwilini.
Kitunguu maji kina viambato vinavyosaidia kupunguza msongamano wa damu kwenye mishipa na kuongeza mtiririko wake kuelekea sehemu za siri za mwanaume, jambo linalosaidia kusimama vizuri kwa uume.

3) Huongeza Stamina Na Nguvu Za Mwili.
Kwa kuwa kitunguu maji kina virutubisho kama vitamin C, B6, madini ya chuma na foliki asidi (folate), husaidia kupunguza uchovu na kuongeza nguvu mwilini, hivyo mwanaume anapata uwezo wa kufanya tendo la ndoa bila kuchoka haraka.

4) Huimarisha Ubora Na Wingi Wa Shahawa.
Kitunguu maji kina madini ya zinki na antioxidants yanayosaidia kulinda mbegu za kiume dhidi ya uharibifu na kuongeza uwezo wa mwanaume kutungisha mimba.


Jinsi ya Kutumia Kitunguu Maji kuboresha Nguvu za Kiume:
Zifuatazo ni njia za kutumia kitunguu maji katika kuboresha kuboresha nguvu za kiume:
1) Juisi Ya Kitunguu Maji.
- Chukua kitunguu maji 1-2, menya, saga kupata juisi yake.
- Changanya na kijiko kimoja cha asali.
- Kunywa mchanganyiko huo (juisi ya kitunguu maji+asali) mara moja kwa siku, hasa usiku kabla ya kulala.
2) Kuchanganya Na Asali.
- Kata vipande vidogo vidogo vya kitunguu maji, weka kwenye glasi ya maji vuguvugu, ongeza asali kisha unywe mchanganyiko huo.
HITIMISHO:
Usitumie kupita kiasi (zaidi ya vitunguu 2 vikubwa kwa siku) kwani huweza kusababisha gesi tumboni na kiungulia.
Epuka kama una vidonda vya tumbo au mzio wa kitunguu.
Epuka kutumia kitunguu maji kibichi sana ikiwa una tatizo la kutoa harufu mbaya mdomoni (halitosis).
Kwa matokeo mazuri, tumia kitunguu maji pamoja na kuishi mtindo bora wa maisha ikiwemo kula lishe bora, kufanya mazoezi na kuepuka matumizi ya pombe na sigara kupita kiasi.
Kwa kifupi, kitunguu maji ni chakula cha asili chenye mchango wa kweli kwenye kuimarisha nguvu za kiume na afya ya mfumo wa uzazi wa mwanaume.
Leave a Reply