Parachichi:
Parachichi lina faida nyingi muhimu kwa afya ya wanawake, kutokana na utajiri wa virutubisho na mafuta mazuri ambayo hutoa mchango mkubwa kwa ustawi wa mwili.

Leo katika mada yetu ya blogu hii tutazungumzia baadhi ya faida za parachichi kwa mwanamke. Ungana nami katika kuchambua faida hizi.
1) Kuimarisha Kinga Ya Mwili.
Vitamini C, B, na E kutoka kwenye parachichi huimarisha mfumo wa kinga hivyo kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa mbalimbali kwa wanawake.

2) Huimarisha Ngozi Na Nywele.
Parachichi lina vitamini E, C na mafuta ya asili yanayosaidia ngozi kuwa laini, yenye unyevunyevu na kupunguza mikunjo. Pia husaidia nywele kukua kwa afya, kupunguza kukatika na kuongeza mng’ao.

3) Kuboresha Afya Ya Moyo.
Mafuta ya parachichi yanaweza kusaidia kupunguza kiwango cha cholesterol mbaya (Low Density Lipopritein) na kuongeza cholesterol nzuri (High Density Lipoprotein), ambayo inasaidia kuboresha afya ya moyo kwa mwanamke.

4) Afya Ya Mfumo Wa Uzazi Na Ujauzito.
Parachichi lina foliki asidi (folate) kwa kiwango kikubwa, kirutubisho muhimu kwa wanawake hasa wajawazito kwani husaidia kuzuia kasoro za kuzaliwa kwa mtoto, hususan kwenye ubongo na uti wa mgongo (neural tube defects). Pia, linaweza kusaidia kupunguza hatari ya kuharibika kwa mimba (miscarriage).

5) Kuzuia Tatizo La Kukosa Choo.
Parachichi lina kiasi kikubwa cha nyuzinyuzi (fibers), ambazo husaidia katika kumeng’enya chakula na kuzuia tatizo la kukosa choo, ambalo ni kawaida kwa wanawake wajawazito.

6) Afya Ya Mifupa.
Parachichi lina vitamini K, foliki asidi (folate), na madini muhimu kama vile shaba yanayochangia kuimarisha mifupa na kuzuia matatizo kama vile osteoporosis ambayo yanawakumba wanawake hasa wa umri mkubwa.

7) Kuboresha Ufyonzaji Wa Virutubisho.
Mafuta yenye afya ya parachichi husaidia mwili kufyonza (absorbs) vitamini mumunyifu (fat soluble vitamins) A, D, E, na K kutoka vyakula vingine, hivyo kuongeza manufaa ya lishe kwa ujumla.

HITIMISHO:
Kwa kuzingatia faida hizo hapo juu, parachichi ni tunda muhimu na salama kuongeza kwenye lishe ya kila siku ya mwanamke, hasa wajawazito, wale wanaotaka afya bora ya ngozi na nywele, na wote wanaotaka kujikinga dhidi ya magonjwa sugu. Ni muhimu tu kulila kwa kiasi sahihi kutokana na kalori zake.
Leave a Reply