Punyeto kwa mwanamke ni tendo la kujistarehesha kwa njia ya kujichua au kujisisimua kingono bila kushirikiana na mtu mwingine (mwanaume).
Ingawa punyeto ni tabia inayozungumziwa na kujulikana kwa wanaume, wanawake pia hushiriki katika tabia hii.
Kama ilivyo kwa wanaume, punyeto kwa wanawake pia inaweza kuwa na madhara au faida kulingana na jinsi inavyofanywa.
Leo katika mada yetu ya blogu hii tutazungumzia baadhi ya madhara ambayo yanaweza kutokea kwa wanawake kutokana na punyeto. Ungana nami katika kuchambua madhara haya.
1) Maambukizi Ukeni.
Matumizi ya mikono au vifaa visivyo safi wakati wa kupiga punyeto vinaweza kuingiza bakteria kwenye uke, na kusababisha maambukizi ukeni kama vile maambukizi ya njia ya mkojo (UTI) au maambukizi ya fangasi ukeni (vaginal yeast infection).
2) Uke Mlegevu.
Kujichua mara nyingi kwa mwanamke kunaweza kusababisha uke kuwa mlegevu, hali ambayo inaweza kuathiri hisia wakati wa tendo la ndoa.
3) Maumivu Ya Via Vya Uzazi.
Ikiwa punyeto inafanywa na mwanamke mara kwa mara na kwa nguvu kupita kiasi, inaweza kusababisha maumivu kutokana na msuguano mwingi katika via vya uzazi mfano clitoris kwa muda mrefu.
4) Kupungua Kwa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa Na Mwenza.
Wanawake wanaweza kukosa hisia au hamu ya kushiriki tendo la ndoa na wenzi wao kutokana na kuzoea raha ya punyeto, ambayo inaweza kuathiri uwezo wao wa kufika kileleni wakati wa ngono.
5) Kupoteza Furaha Ya Tendo La Ndoa.
Baadhi ya wanawake wanaweza kupata hali ya kutoridhishwa na mwenza wao baada ya kuzoea aina fulani ya raha wanayoipata kupitia punyeto.
6) Kujisikia Hatia Au Aibu.
Katika baadhi ya jamii au dini, punyeto huonekana kama jambo lisilokubalika, na hivyo inaweza kusababisha hisia za hatia au aibu kwa mwanamke. Hii inaweza kusababisha hali ya kiakili ya kujihukumu au kujiona kuwa na makosa, ambayo inaweza kuathiri ustawi wa kisaikolojia.
7) Uraibu (Addiction).
Tabia ya kujichua (punyeto) pia inaweza kupelekea mwanamke kupata uraibu (addiction), hali ambapo mwanamke anakuwa na hitaji la mara kwa mara la kujichua, kiasi kwamba tabia hii inaingilia au kuathiri maisha ya kila siku, kazi, au mahusiano.
HITIMISHO:
Kwa ushauri na tiba ya magonjwa ya afya ya uzazi wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487.
Ni mimi mwenye kujali afya yako Dr. Isaya Febu, nikutakie siku njema.
Leave a Reply