Madhara Ya Kufanya Mapenzi Ukiwa Period.

Kufanya mapenzi wakati wa period ni suala lenye mjadala mkubwa katika masuala ya afya. Kuna baadhi ya madhara na hatari zinazoweza kutokea kwa mwanaume (na pia kwa mwanamke) kutokana na kufanya mapenzi wakati wa period.

Kufanya Mapenzi

Leo katika mada yetu ya blogu hii tutazungumzia madhara ya kufanya mapenzi wakati wa period kwa wanaume na wanawake. Ungana nami katika kuchambua madhara haya.

A) Madhara Kwa Wanawake:

Yafuatayo ni baadhi ya madhara yanayoweza kutokea kwa wanawake kutokana na kufanya mapenzi wakati wa period ambayo ni pamoja na:

1) Maumivu Na Kutokwa Na Damu Nyingi Zaidi.

Wakati wa period, baadhi ya wanawake wanaweza kuwa na maumivu zaidi ya tumbo (dysmenorrhea) na kutokwa na damu nyingi zaidi.

Kufanya mapenzi wakati huo kunaweza kuongeza maumivu na kusababisha kutokwa na damu nyingi zaidi.

2) Hatari Ya Kupata Maambukizi.

Kwa wanawake, kufanya mapenzi wakati wa period kunaweza kuongeza hatari ya kupata maambukizi ya uke au njia ya mkojo kutokana na mlango wa uzazi (cervix) kuwa wazi zaidi kwa bakteria ikiwa wapenzi wao wana maambukizi. Mfano wa maambukizi hayo ni pamoja na Pelvic inflammatory Disease (PID), maambukizi ya zinaa (STIs) n.k

3) Saratani Ya Shingo Ya Kizazi.

Kufanya mapenzi wakati wa period kunaweza kuongeza hatari ya kuambukizwa virusi vya HPV (Human Papilloma Virus), ambavyo vinasababisha saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake.

4) Kuziba Kwa Mirija Ya Uzazi.

Kwa wanawake, kufanya mapenzi wakati wa period kunaweza kuongeza hatari ya kuziba kwa mirija ya uzazi (fallopian tubes), hali ambayo inaweza kusababisha ugumba au matatizo ya uzazi.

5) Hatari Ya Kupata Ujauzito.

Ingawa ni nadra, kuna hatari ya kupata mimba wakati wa hedhi. Manii (sperms) inaweza kuishi kwa siku kadhaa (mpaka siku 5) ndani ya mwili wa mwanamke, na inawezekana kutokea ovulation (kutoa yai) mapema.

B) Madhara Kwa Wanaume:

Yafuatayo ni baadhi ya madhara yanayoweza kutokea kwa wanaume kutokana na kufanya mapenzi wakati wa period ambayo ni pamoja na:

1) Hatari Ya Kupata Maambukizi.

Wanaume wanaweza kuwa katika hatari ya kupata maambukizi ya zinaa wakati wa kufanya mapenzi kipindi cha hedhi, ikiwa wapenzi wao wana hayo maambukizi.

2) Matatizo Ya Tezi Dume.

Kwa wanaume kufanya mapenzi wakati wa period kunaongeza hatari ya damu ya hedhi kuingia kwenye tezi dume, hali ambayo inaweza kusababisha ugumba au matatizo ya tezi dume mfano prostatitis.

3) Athari Ya Kisaikolojia.

Baadhi ya wanaume wanaweza kuhisi wasiwasi au kutojisikia vizuri kufanya mapenzi wakati wa period kutokana na kuvuja damu, harufu, au maumivu ambayo wapenzi wao wanaweza kuhisi.

4) Tatizo La Uume Kusimama Lege Lege.

Wakati wa kufanya mapenzi kipindi cha hedhi, uchafu unaotoka ukeni ukiingia kwenye mishipa ya damu ya uume  unaweza kupelekea tatizo la uume kusimama lege lege, hali ambayo hujulikana kwa kitaalamu kama erectile dysfunction.

Soma pia hizi makala:

HITIMISHO:

Kufanya mapenzi wakati wa period kunaweza kufanyika kwa maelewano kati ya wenzi wawili na tahadhari sahihi, lakini ni muhimu kuelewa hatari zinazoweza kutokea na kuchukua hatua za kuzuia madhara yoyote ya kiafya ikiwemo matumizi ya kinga kama vile kondomu ili kupunguza hatari za maambukizi.