Madhara Ya Kufanya Mapenzi Wakati Wa Hedhi Kwa Mwanaume.

Kufanya mapenzi wakati wa hedhi ni suala lenye mjadala mkubwa katika masuala ya afya. Kuna baadhi ya madhara na hatari zinazoweza kutokea kwa mwanaume (na pia kwa mwanamke) kutokana na kufanya mapenzi wakati wa hedhi.

Kufanya Mapenzi

Leo katika mada yetu ya blogu hii tutazungumzia madhara ya kufanya mapenzi wakati wa hedhi kwa wanaume . Ungana nami katika kuchambua madhara haya.

1) Hatari Ya Kupata Maambukizi.

Wanaume wanaweza kuwa katika hatari ya kupata maambukizi ya zinaa wakati wa kufanya mapenzi kipindi cha hedhi, ikiwa wapenzi wao wana hayo maambukizi.

2) Matatizo Ya Tezi Dume.

Kwa wanaume kufanya mapenzi wakati wa hedhi kunaongeza hatari ya damu ya hedhi kuingia kwenye tezi dume, hali ambayo inaweza kusababisha ugumba au matatizo ya tezi dume mfano prostatitis.

3) Athari Ya Kisaikolojia.

Baadhi ya wanaume wanaweza kuhisi wasiwasi au kutojisikia vizuri kufanya mapenzi wakati wa hedhi kutokana na kuvuja damu, harufu, au maumivu ambayo wapenzi wao wanaweza kuhisi.

4) Tatizo La Uume Kusimama Lege Lege.

Wakati wa kufanya mapenzi kipindi cha hedhi, uchafu unaotoka ukeni ukiingia kwenye mishipa ya damu ya uume  unaweza kupelekea tatizo la uume kusimama lege lege, hali ambayo hujulikana kwa kitaalamu kama erectile dysfunction.

HITIMISHO:

Kufanya mapenzi wakati wa hedhi kunaweza kufanyika kwa maelewano kati ya wenzi wawili na tahadhari sahihi, lakini ni muhimu kuelewa hatari zinazoweza kutokea na kuchukua hatua za kuzuia madhara yoyote ya kiafya ikiwemo matumizi ya kinga kama vile kondomu ili kupunguza hatari za maambukizi.