Jinsi Ya Kuongeza Damu Kwa Haraka Kwa Mjamzito.

Kuongeza damu kwa haraka kwa mjamzito ni muhimu ili kuhakikisha afya yake na mtoto anayekua tumboni. Upungufu wa damu, hasa wa madini ya chuma (anemia), ni tatizo linaoathiri wanawake wengi wakati wa ujauzito. 

Ili kusaidia kuongeza damu haraka, ni muhimu kuzingatia lishe yenye virutubisho sahihi na kufuata ushauri wa daktari.

mjamzito

Baadhi ya njia za kuongeza damu kwa mjamzito ni pamoja na:

1) Kula Vyakula Vyenye Madini Ya Chuma.

Madini ya chuma husaidia mwili kuzalisha hemoglobini, sehemu muhimu ya seli nyekundu za damu. Vyakula vyenye madini ya chuma ni pamoja na:

  • Nyama nyekundu (mfano nyama ya ng’ombe au mbuzi)
  • Maini
  • Mboga za majani kama vile spinachi na sukuma wiki
  • Maharage, njegere, na kunde
  • Karanga na mbegu za maboga, mbegu za almond

2) Matumizi Ya Virutubisho Vya Madini Ya Chuma.

Daktari anaweza kumuandikia mama mjamzito vidonge vya kuongeza madini ya chuma (iron supplements). Hivi vidonge ni muhimu hasa kwa wajawazito wenye upungufu mkubwa wa damu.

ferrous sulphate

3) Kula Vyakula Vyenye Vitamini C.

Vitamini C husaidia mwili kufyonza madini ya chuma vizuri zaidi. Kula vyakula vyenye vitamini C kama vile:

  • Machungwa
  • Mapapai
  • Nyanya

4) Kuepuka Vyakula Vinavyopunguza Unyonyaji Wa Madini Ya Chuma.

Baadhi ya vyakula na vinywaji kama vile chai na kahawa vinaweza kuzuia ufyonzaji wa madini ya chuma. Ni vizuri kuepuka au kupunguza matumizi ya vyakula hivi, hasa wakati wa kula vyenye madini ya chuma.

kahawa

5) Kula Vyakula Vyenye Asidi Ya Foliki.

Asidi ya foliki ni muhimu katika utengenezaji wa seli nyekundu za damu. Vyanzo vya asidi ya foliki ni pamoja na:

  • Spinachi
  • Karoti
  • Parachichi
  • Mayai

6) Virutubisho Vya Asidi Ya Foliki.

Wajawazito wanashauriwa kutumia virutubisho vya asidi ya foliki kwani ni muhimu kwa afya ya mama na mtoto.

folic acid tabs/

7) Kunywa Maji Ya Kutosha.

Maji ni muhimu kwa usafirishaji wa virutubisho mwilini, hivyo ni muhimu kunywa maji ya kutosha kusaidia ufyonzaji wa virutubisho vyenye chuma.

maji

Soma pia hii makala: Mama Mjamzito: Mambo 7 Muhimu Ya Kuzingatia.

HITIMISHO:

Ni muhimu kumwona daktari mara kwa mara ili kufuatilia kiwango cha damu na kupata ushauri wa kitaalamu ikiwa utahitaji matibabu zaidi kama vile kuongezewa damu.

Kwa kufanya haya, mama mjamzito anaweza kuongeza kiwango cha damu na kujikinga dhidi ya upungufu wa damu.