Kujichua Kwa Wanawake:
Kujichua kwa wanawake au kwa lugha ya kitaalamu female masturbation, ni kitendo cha mwanamke kujisisimua kingono mwenyewe kwa kutumia mikono au vifaa (sex toys) ili kupata raha ya kimapenzi au kufika kileleni (orgasm).


Baadhi ya wanawake hufanya kitendo hicho kwa sababu mbalimbali kama vile:
1) Kupunguza Msongo Wa Mawazo (Stress).
Kujichua hutoa homoni za furaha kama endorphins na dopamine, zinazosaidia kuondoa msongo wa mawazo na kuongeza furaha.
2) Kuboresha Usingizi.
Baada ya kufika kileleni kutokana na kujichua, mwili hupata utulivu unaosaidia kulala kwa urahisi.
3) Kujitambua Kimwili.
Mwanamke hujifunza ni sehemu zipi zinamletea raha zaidi.
Athari Za Kujichua Kwa Mwanamke:
Athari za kujichua kwa mwanamke ni pamoja na:
1) Kujisikia Hatia Au Aibu.
Katika baadhi ya jamii au dini, kujichua kwa mwanamke huonekana kama jambo lisilokubalika, na hivyo inaweza kusababisha hisia za hatia au aibu kwa mwanamke. Hii inaweza kusababisha hali ya kiakili ya kujihukumu au kujiona kuwa na makosa, ambayo inaweza kuathiri ustawi wa kisaikolojia.
2) Kupungua Kwa Hamu Ya Tendo La Ndoa Na Mwenza.
Mwanamke anaweza kukosa hisia au hamu ya kushiriki tendo la ndoa na mwenzi wake kutokana na kuzoea raha ya kujichua, ambayo inaweza kuathiri uwezo wake wa kufika kileleni wakati wa ngono.
3) Kupoteza Furaha Ya Tendo La Ndoa.
Baadhi ya wanawake wanaweza kupata hali ya kutoridhishwa kingono na wenza wao baada ya kuzoea aina fulani ya raha wanayoipata kupitia kujichua.
4) Uraibu (Addiction).
Tabia ya kujichua pia inaweza kupelekea mwanamke kupata uraibu (addiction), hali ambapo mwanamke anakuwa na hitaji la mara kwa mara la kujichua, kiasi kwamba tabia hii inaingilia au kuathiri maisha ya kila siku, kazi, au mahusiano.
5) Maumivu Ya Via Vya Uzazi.
Ikiwa kujichua kunafanywa na mwanamke mara kwa mara na kwa nguvu kupita kiasi, inaweza kusababisha maumivu kutokana na msuguano mwingi katika via vya uzazi mfano clitoris (kinembe) kwa muda mrefu.
6) Maambukizi Ukeni.
Matumizi ya mikono au vifaa visivyo safi wakati wa kujichua vinaweza kuingiza bakteria kwenye uke, na kusababisha maambukizi ukeni kama vile maambukizi ya njia ya mkojo (UTI) au maambukizi ya fangasi ukeni (vaginal yeast infection).
HITIMISHO:
Kwa msaada wa kisaikolojia kutokana na kuathirika na tabia ya kujichua kwa muda mrefu (unatamani kuacha tabia hiyo lakini unashindwa) wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487.
Ni mimi mwenye kujali afya yako Dr. Isaya Febu, nikutakie siku njema.
Leave a Reply